Header Ads

TAMKO LA MUHESHIMIWA WAZIRI WA HABARI UTALII NA MAMBO YA KALE KATIKA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI DUNIANI MEI 3 2018



Ulimwengu unaadhimisha siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani.Maadhimisho hayo yanafanyika kesho jijini Accra Ghana yakiongozwa na shirika la elimu sayansi na utamaduni la umoja wa mataifa UNESCO
Ni siku ambayo dunia inatathmini hali ya uhuru wa vyombo vya habari duniani kote ambapo inatolewa michango ya kutetea vyombo vya habari vinavyokabiliana na mashambulizi pamoja na kuwakumbuka waandishi wa habari waliopoteza maisha yao wakiwa kazini.
Kila mwaka zaidi ya waandishi maadhimisho 100 ya kitaifa yanafanyika kuiadhimisha siku hii na shirika la elimu sayansi na utamaduni la umoja wa mataifa UNESCO ndilo linaloongoza maadhimisho hayo katika kila pembe ya dunia.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni ‘wajibu wa Uongozi Vyombo vya habari,haki na utawala wa sheria.
Ndugu wananchi serikali ya mapinduzi Zanzibar inatambuwa umuhimu wa siku hii ambayo ilitangazwa na baraza kuu la umoja wa mataifa mwaka 1993 kufuatia pendekezo la mkutano mkuu wa 26 wa UNESCO  mwaka 1991 lililotokana na azimio la windhock la waandishi wa habari wa afrika la mwaka huo huo kuhusu maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya habari
Ndugu wananchi azimio hilo vile vile liliridhia kuanzishwa kwa taasisi ya vyombo vya habari kusini mwa afrika MISA Ambayo wote tunajuwa mchango wake katika  kupigania uhuru wa vyombo vya habari maadili na weledi katika tasnia ya uandishi wa habari.

Siku ya uhuru wa vyombo vya habari mwaka huu inaonesha uhusiano kati ya serikali kwa upande mmoja na uhuru wa vyombo vya habari haki na utawala wa sheria.
Ndugu wananchi sekta ya ahbari ni sekta za huduma za jamiihapa nchini. Sekta hii inatowa huduma ambayo ni haki ya msingi ya raia kama inavyotamkwa kwenye katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984. Ibara ya 18 ya katiba inasema
1. Kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake na kutafuta kupokea na kutoa habari na dhana zozotekupitia chombo chochote bila ya kujali mipaka ya nchi na pia ana uhuru wa mawasiliano yakekutoingilia kati.
2. Kila raia ana haki ya kupewa taarifa wakakti wowote kuhusu  matukio nchinina duniani kote ambayo ni muhimu kwa maisha ya na shughuli za wananchi na pia ni juu ya masuala muhimu kwa jamii. Aidha kutoa na kupokea habari kunatambuliwa duniano kote kuwa ni moja ya haki za binaadamu.
Ndugu wananchi umoja wa mataifa na umoja wa afrika zina matamko rasmi ambayo serikali imeridhia kuhusu haki ya kupokea na kutoa habari.
Haki hii,kama zilivyo haki nyengine zote hutolewa kwa kuzingatia wajibu wa kila raia kwa jamii na uhuru binafsi wa binaadamu.
Ndugu wananchi,serikali ya mapinduzi Zanzibar itaendelea kuheshimu na kukuza uhuru wa vyombo vya habari na uhuru wa kujielezea kama ilivyoelekeza katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.
Ndugu wananchi kuna mafanikio chanya kwa upande wa vyanzo vya habari hapa Zanzibar hali ilivyo leo tofauti sana na ilivyokuwa huko nyuma, serikali imekuwa ikihimiza maafisa wakuu kutoa ushirikiano kwa vyombo vya habari.
Ndugu wananchi mara kadhaa tumemsikia Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi, mheshimiwa Dk,Ali Mohd Sheni akihimiza viongozi wenzake serikalini kushirikiana kwa karibu na waandishi wa habari.

Ndugu wananchi, Ripoti mbali mbali zile za waandishi wasiokuwa na mipaka {Repoters Without Borders}, vyama vya kutetea waandishi wa habari vinasema kwamba uhuru na usalama wa waandishi wa habari umeonekana kuwa mdogo na usiowapa uhakika wa kufanya kazi zao kwa ufanisi katika mataifa kadhaa.
Ndugu wananchi, hali hiyo ni tofauti  sana na hapa Zanzibar ambapo ukisoma katika magazeti ukisikiliza redio ukitazama televisheni majarida mitandao ya kijamii serikali imekuwa ikikosolewa wazi wazi.
Wakati mwengine waandishi wamevuka mipaka kwa kuinanga serikali, lakini hakuna aliyechukuliwa hatua za kisheria au kutishwa, sisemi sasa Serikali ifanye kinyume chake la hasha lakini naonesha jinsi gani serikali ilivyo na uvumilivu kwa kujenga jamii yenye kuvumiliana kimawazo.
Ndugu wananchi, wakati huu tukiadhimisha siku ya uhuru wa vyombo vya habari sina budi kumshukuru kwa dhati rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Mheshimiwa Dk Ali Mohd Sheni kwa uamuzi wake wa kuviimarisha vyombo vya habari vya serikali.
Mageuzi makubwa katika kulijengea uwezo Shirika La Utangazaji Zanzibar mikutano yake na waandishi wa habari  pamoja na uwazi,kusimamia misingi ya utawala bora ushirikishwaji wa vyombo vya habarikatika shuhuli mbalimbali za serikali na mengineyo ni thamira tosha ya serikali katika kukuza uhuru wa vyombo vya habari.

Ndugu waandishi wa habari nimalizie kwa kusema  kuwa suala moja ni muhimu katika hayo yote  ni jukumu la uandishi wa habari unaozingatia ueledi, uzalendo heshima kwa jamii na umuhimu wa kuwalinda wale ambao wanahusika katika taaluma hii inayohudmia umma.
Asanteni.

No comments:

Powered by Blogger.