Rais Dkt. John Magufuli
amesema amesikitishwa na vitendo vya Mabalozi kushindwa kutekeleza
maagizo yake aliyowapa ya kumpa taarifa juu ya utendaji kazi wao na
manufaa ambayo Tanzania imeyapata kwa uwepo wa kila Balozi katika nchi
aliyopangiwa kila robo mwaka.
Dkt.
Magufuli ametoa kauli hiyo leo Mei 10, 2018 wakati alipokuwa
anazungumza mara baada ya kumaliza kumuapisha Mhe. Alphayo Japani Kidata
kuwa Balozi wa Tanzania nchini Canada na Bw. Msalika Robert Makungu
kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora, Ikulu Jijini Dar es Salaam na
kuwataka viongozi hao kwenda kuchapa kazi kwa juhudi na maarifa na kwa
manufaa ya Taifa na sio kufanya mambo ndivyo sivyo.
"Nataka nijue katika kipindi ambacho Mhe. Balozi
ameteuliwa kuiwakilisha Tanzania katika nchi fulani, nchi imenufaikaje
na uwepo wake kwenye nchi ile?. Kuteuliwa sawa lakini sio lazima ukae
katika ubalozi huo kwa kipindi chote ulichopangiwa, ukishindwa kuleta
manufaa unarudishwa na huko anapangiwa mtu mwingine atayeleta manufaa
kwa nchi", amesema Rais Magufuli.
Kwa upande mwingine, Rais Magufuli ameipongeza Wizara ya Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwa kufanya kazi nzuri katika
sekta ya Elimu na Afya
No comments: