Anayempinga Rais Magufuli anatatizo - Makonda
“Niendelee kuwasihi wananchi, yeyote yule atakaye waambia hakuna chochote kinachofanyika na kutendeka ujue kwamba ni tatizo la akili au ameuamua kukaa upande wa shetani kwa kupinga hata mambo mema yanayofanywa na Rais Magufuli, unampinga kwa kujenga stendi ya Ubungo ya kukupatia zaidi ya bilioni 50? unampinga kwa kujenga Standard Gauge? unampinga kwa kuleta Bombardier? Au unampinga kwa kupanua bandari?", amesema Makonda.
Makonda ameongeza kuwa serikali kuu kupitia Wizara ya Tamisemi na Wizara ya Fedha na Mipango imetenga kiasi cha shilingi bilioni 250 kwaajili ya kutekeleza miradi mbalimbali katika jiji la Dar es salaam.
Mkuu mkoa pia alielezea baadhi ya miradi mbalimbali ambayo serikali imetekeleza na ile ambayo ipo mbioni kukamilika katika mkoa wa Dar es salaam ikiwemo, upanuzi wa bandari ya Dar es salaam, miradi ya ujenzi wa barabara, kituo cha mabasi Mbezi, Soko la Kisutu, Mradi wa mabasi ya mwendokasi awamu ya pili.
Makonda aliwasihi wakurugenzi waliopo katika jiji la Dar es salaam ambao ni wasimamizi wakuu wa fedha, kutokuwa na uwoga wa kuchukua hatua kwa mtu yeyote kwasababu wao ni wateule wa Rais John Magufuli.

No comments: