"Wanachama wetu wanaugua" - Msigwa
Msigwa
ametoa kauli hiyo leo asubuhi Mei 04, 2018 baada ya moja ya video yake
kuendelea kusambaa kwa kasi zaidi kwenye mitandao ya kijamii
ikimuoonyesha akimsifia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli kuwa katika kipindi chake amekuwa hajali vyama licha
ya yeye kuitolea ufafanuzi wa kina siku ya Jana Mei 03, 2018.
"Ufafanuzi wangu bado haueleweki na ni heshima kuzingatia maumivu yenu kwa mkanganyiko huu. Nagundua rafiki zangu na wanachama wetu wanaugua. Basi niseme nini?, naomba nisameheni sana. 'The cause we are fighting for is more important than my personality. I take full responsibility", amesema Msigwa.
Tokea kuenea kwa video hiyo, wanachama wa CHADEMA wamekuwa wakitoa maneno mengi juu ya Mbunge huyo huku wengine wakifika mbali zaidi kuwa huenda nae anataka kutimukia CCM.

No comments: