Yanga yawasubirisha wanachama wake
Hayo
yamebainishwa na Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa na kusema kabla
ya mkutano huo wanachama wa timu hiyo nchi nzima wanapaswa kuweka kadi
zao za benk au zile za kawaida zikiwa hai kwa maana ya kulipia ili kila
mtu aweze kutumia haki ya msingi kuweza kurekebisha mapungufu ndani ya
klabu kwa kuziba nafasi za viongozi zilizowazi kwa sasa.
"Sababu zilizofanya kupeleka mkutano huo mbele ni kutokana na hapa kati kulikuwa na mechi za Ligi ambazo zilikuwa karibu karibu sana na awali tulitaka tufanye mkutano Mei 05 lakini tukaletewa ratiba ya mechi na Mbao FC na baadaye ndipo tukapata ratiba ya kombe la Shirikisho hivyo tunaamini sababu hizo ni za msingi na tusingeweza kuchanganya masuala ya mkutano na mechi", amesema Mkwasa.
Kwa upande mwingine, Yanga inatarajia kushuka dimbani siku ya Jumapili Mei 6, 2018 nchini Algeria kuminyana na USM Alger kwenye mchezo wa kwanza hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika.

No comments: