Header Ads

HUJAFA HUJAUMBIKA

HUJAFA HUJAUMBIKA: Mwanamama Sidonia Ntibashigwa maarufu kama Mama Sophia, mkazi wa Machimbo ya zamani, Salasala Mbuyuni amemshukuru Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan kwa kumpatia kiti cha magurudumu (wheel chair) kitachokuwa msaada wa kuendelea na shughuli zake za hapa na pale.
Mama Sophia kwa sasa ni mlemavu baada ya kupata ajali ya kugongwa na roli Mei 28, 2016 katika maeneo ya Mbuyuni, Salasala jijini Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa kumkabidhi kiti hicho, Msaidizi wa Makamu wa Rais upande wa Siasa Nehemia Mandia amesema Makamu wa Rais aliguswa na suala la mwanamama huyo baada ya kusoma katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.

No comments:

Powered by Blogger.