Teknolojia mpya upasuaji mgongo yaanza Muhimbili
Madaktari wa Taasisi ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (MOI) Muhimbili,
jijini Dar es Salaam wakishirikiana na wataalamu kutoka Hospitali ya
BLK- India wamefanya upasuaji kwa wagonjwa waliodhohofika migongo kwa
kutumia teknolojia mpya (minimally invasive surgery) inayomwezesha
mgonjwa kurudi katika hali yake ya kawaida ndani ya wiki moja.
Kwa mujibu wa daktari bingwa wa MOI, Profesa Joseph Kahamba, upasuaji huo ni wagonjwa waliodhoofu migongo ambapo upasuaji huathiri mishipa ya fahamu. Mtaalamu kutoka India, Daktari Puneet Girdhan alisema upasuaji huo hauhitaji mgonjwa kuongezewa damu na hufanyika kwa muda mfupi usiozidi saa tatu.
Aidha, teknolojia hiyo inamwezesha mgonjwa kuruhusiwa ndani ya siku mbili tofauti na upasuaji wa zamani ambapo mgonjwa alilazimika kukaa hospitali kwa muda usiopungua wiki moja.
Baadhi ya dalili za kudhoofu kwa mgongo ni pamoja maumivu makali ya mgongo, ganzi kwenye miguu pamoja na uchovu unamfanya mgonjwa asiweze kutembea muda mrefu bila kupumzika. "Kuchakaa kwa mifupa hujitokeza katika umri wa miaka 28 hadi 30 lakini athari zake huanza kujitokeza kwenye umri wa miaka 50 hadi 60.
Ukigundulika mapema mgonjwa atatibiwa kwa dawa na kupona kabisa. Upasuaji kama huu ni kwa mgonjwa aliyechelewa kujua tatizo, hivyo tunashauri watu kupima afya zao mara kwa mara," alisema Profesa Kahamba. Sambamba na hilo, mtaalam huyo alishauri mazoezi, kuwa na uzito unaoendana na urefu pamoja na kulalia godoro gumu.

No comments: