Header Ads

Mama Unju Afunguka Kuhusu Alikiba na Matunzo ya Watoto Wake.

Baada ya kusambaa kwa tetesi nyingi katika mitandao ya kijamii kuhusu tabia ya Alikiba kutelekeza watoto na kwamba hatoi matunzo kwa watoto wake, mmoja ya wanawake aliobahatika nae kupata mtoto aliejulikana kama Mama Unju ambae ni amma wa mtoto wake wa kiume amefunguka na kumkingia kifua Alikiba na kusema kuwa wanawale hao wanataka kurudiana na Alikiba lakini wanakosa njia ya kufanya hivyo.
Mama Unju anasema kuwa Alikiba hana tabia hiyo kwa watoto wake na kwamba mwanamke aliezusha hivyo amekuwa akitamani kila siku kurudiana kimapenzi na Alikiba lakini ali amekuwa akimkwepa na ndio maana anatumia mtoto kama kigezo cha kurudisha mahusiano yake.


Mama Unju aliendelea na kufunguka kuwa kwa wanawake wote ambao wamezaa na Alikiba , sio tabia nzuri kutumia watoto wao kutaka kurudiana na Alikiba au kutumia watoto wao ili kujinufaisha na familia nzima, wanatakiwa kushukuru pale ambapo wanapata matunzo ya watoto wao na sio kulisha familia nzima na kuwataka kukubaliana na matokea kuwa hawapo tena na Alikiba na kupambana na hali zao kama vile yeye alivyokubali kuwa walishatengana na Alikiba na maisha lazima yaendelee.
Kwa ushauri zaidi ambao Mama Unju ameutoa kwa alikiba na wasanii wengine ni kwamba,wanatakiwa kuwa makini sana kuangalia wanawake wanaotoka nao kimapenzi kwa sababu kuna baadhi ya wadada wamekuwa hawajielewi na wamekuwa wakifanya vitu kwa kukomoa.

No comments:

Powered by Blogger.