Kilichoendelea Mahakamani Katika Kesi ya Rugemariila wa ESCROW
MAHAKAMA
ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam jana iliipiga kalenda kesi
inayomkabili mfanyabiashara James Rugemalila na mwenzake hadi Machi 16.
Rugemarila
na mfanyabiashara Harbinger Sethi wanakabiliwa na mashtaka 12 ya
uhujumu uchumi, kutakatisha fedha na kuisababisha Serikali hasara ya
dola za Marekani 22,198,544.60 na Sh. bilioni 309.
Awali
Wakili wa Serikali Mwandamizi, Leornad Swai alidai upelelezi wa kesi
hiyo bado haujakamilika na upande wa Jamhuri uliomba tarehe nyingine ya
kutajwa.
Hakimu
Shaidi alisema kesi hiyo itatajwa tena Machi 16 na washtakiwa
wataendelea kukaa mahabusu. Walipopandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza
Julai, mwaka huu upande wa Jamhuri ulidai:
Kati
ya Oktoba 18, 2011 na Machi 19, 2014 jijini Dar es Salaam Sethi na
Rugemalira walikula njama katika nchi za Afrika Kusini, Kenya na India
ili kutenda kosa.
Ulidai
katika shitaka la pili kati ya Oktoba 8,2011 na Machi 19,2014 jijini
Dar es Salaam wakiwa siyo watumishi wa umma walishirikiana na watumishi
wa umma kutekeleza mtandao huo wa uhalifu kwa lengo la kujipatia faida.
Katika
shitaka la tatu linalomkabili Sethi, inadaiwa kuwa Oktoba 10, 2011
katika Mtaa wa Ohio, Ilala Dar es Salaam akiwa na nia ya ulaghai
alighushi fomu namba 14 A ya usajili wa kampuni na kuonyesha kuwa yeye
ni Mtanzania anayeishi kitalu namba 887, Mtaa wa Mrikau, Masaki wakati
akijua sio kweli.
Pia,
Sethi anadaiwa alitoa nyaraka ya kughushi ambayo ni fomu namba 14 A ya
usajili wa kampuni kwa Ofisa msajili wa Kampuni, Seka Kasera kwa nia ya
kuonyesha kwamba yeye ni Mtanzania na mkazi wa Mtaa wa Mrikau, Masaki,
Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Aidha,
Kimaro alidai katika mashitaka ya kujipatia fedha kwamba kati ya
Novemba 28 na 29, 2011 na Januari 23, 2014 katika makao makuu ya Benki
ya Stanbic Kinondoni na Benki ya Mkombozi tawi la Mtakatifu Joseph, kwa
ulaghai washitakiwa hao walijipatia kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BOT),
dola za Marekani 22,198,544.60 na Sh. 309,461,300,158.27.
Pia
washitakiwa wote wanadaiwa kuisababishia serikali hasara ambapo
inadaiwa walitenda makosa hayo Novemba 29, 2013 katika Benki ya Stanbic
tawi la kati, Kinondoni, na kwa vitendo vyao hivyo waliisababishia
serikali hasara ya dola za Marekani 22,198,544.60 na Sh.
309,461,300,158.27.
pande
wa Jamhuri ulidai kati ya Novemba 29, 2013 na Januari 23, 2014 katika
maeneo tofauti Dar es Salaam, kwa pamoja walitenda kosa la kutakatisha
fedha kwa kuchukua fedha kutoka BoT ambazo ni dola za Marekani milioni
22.1 na Sh bilioni 309.4 wakati wakijua fedha hizo ni zao la kujihusisha
na genge la uhalifu.
Katika
shitaka la nane, ulidai kuwa Novemba 29, 2013 katika tawi la kati la
Benki ya Stanbic Tanzania wilaya ya Kinondoni, Sethi alitakatisha fedha
kwa kuchukua kutoka BOT, dola za Marekani milioni 22.1 wakati akijua
fedha hizo zimetokana na zao la kujihusisha na genge la uhalifu.
Aidha,
Sethi anadaiwa kuwa kati ya Novemba 29, 2013 na Machi 14,2014 katika
tawi la kati la Benki ya Stanbic Kinondoni Dar es Salaam alitakatisha
fedha, Sh. bilioni 309.4 kutoka BOT wakati akijua fedha hizo zimetokana
na zao uhalifu.
Katika
shitaka la 10, inadaiwa kuwa Januari 23, 2014 katika Benki ya Mkombozi
tawi la St Joseph Cathedral, Rugemarila alitakatisha fedha ambazo ni Sh.
bilioni 73.5 kutoka kwa Seth wakati akijua fedha hizo zimetokana na zao
la kujihusisha na genge la uhalifu.
Pia
ilidaiwa kuwa Januari 23, 2014 katika Benki ya Mkombozi tawi hilo,
Rugemarila alitakatisha fedha ambazo ni dola za Marekani 22,000,000
kutoka kwa Seth wakati akijua fedha hizo ni zao la uhalifu.
Jamhuri
pia ilidai Januari 28, 2014 katika tawi la Benki ya Stanbic wilaya ya
Kinondoni Sethi alihamisha kwenda Afrika Kusini Rand 1,305,800 kwenda
kwenye akaunti namba 022655123 katika Benki ya Standard Land Rover
Sandton ya Afrika Kusini wakati akijua katika kipindi anahamisha, fedha
hizo zimetokana na zao la kujihusha na genge la uhalifu.
Washtakiwa hao hawakutakiwa kujibu chochote kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi.
Washitakiwa wapo rumande tangu Julai, mwaka jana kwa kuwa mashitaka ya kutakatisha fedha yanayowakabili hayana dhamana.

No comments: