Header Ads

MOTO WAZUA 'TAHARUKI' KOROGWE:

 Moto umeteketeza sehemu ya bweni la wasichana wa Shule ya Sekondari Korogwe na kuwaacha watoto hao katika hali mbaya kufuatia mshtuko wa kupoteza vifaa vyao vyote.
Moto huo ulitokea majira ya saa tatu usiku wakati wanafunzi takribani 40 wanaoishi katika bweni hilo wakiwa darasani wanajisomea.

Hata hivyo licha ya moto huo kutekeza bweni hilo, hakuna madhara ya kimwili kwa upande wa wanafunzi hao isipokuwa kwa wale waliopata mshituko na kuzimia ambao wamelazwa katika Hospitali ya Magunga na Majengo.

Kwa mujibu Wa mashuhuda wa tukio hilo, chanzo cha moto kinadaiwa kuwa ni hitilafu ya umeme.

No comments:

Powered by Blogger.