Header Ads

MUSEVENI AWAWEKA KANDO WAZIRI NA IGP:

 Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametengua uteuzi wa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini humo, Kale Kayihura na waziri wa Ulinzi, Henry Tumukunde.

Generali Kayihura, ambaye ni miongoni mwa washirika waliomsaidia rais Museveni kuingia madarakani mwaka 1986, alikuwa ni afisa mwenye nguvu zaidi katika jeshi hilo la Uganda.
Rais Museveni amemteua msaidizi wake, Okoth Ochola kushika wadhifa huo.
Kupitia ujumbe wake katika ukurasa wa Twitter Rais Museveni, amesema: "Kwa Mamlaka niliyopewa kikatiba, nimemteua Jenerali Elly Tumwiine kuwa waziri wa usalama. Nimemteua pia bwana Okoth Ochola kama Mkuu wa Jeshi la Polisi. Naibu wake atakuwa ni Brigedia Sabiiti Muzeei.”
 

No comments:

Powered by Blogger.