Header Ads

Polisi Kenya watafuta silaha zilizoporwa na wapiganaji wa kundi la Al Shabaab


Polisi nchini Kenya wameimarisha msako dhidi wa wapiganaji wa kundi la Al Shabaab waliovamia kambi mbili za polisi kwenye kaunti ya Mandera, ambapo walipora silaha nyingine na kuwaua polisi watano.
Taarifa iliyotolewa na polisi inasema wapiganaji wa kundi la Al Shabaab walifanya mashambulizi ya kushtukiza kwenye mpaka wa Somalia na kuiba silaha kadhaa.
Taarifa iliyotolewa na polisi siku mbili baada ya shambulizi inasema, polisi wameanzisha msako dhidi ya Jamaa Nuh Abdille, aliyeongoza shambulizi lililosababisha vifo vya polisi watano, na kukimbilia Somalia akiwa pamoja na wenzake.
Taarifa pia inasema wapiganaji wa kundi la Al Shabaab, jumatano walijaribu kufanya shambulizi dhidi ya vituo viwili vya polisi. Polisi walijibu mashambulizi na kufanikiwa kuwakamata wapiganaji watatu wa kundi hilo.

No comments:

Powered by Blogger.