Niyonzima, Mbonde warudi kwa kasi
Afisa Habari wa Klabu ya
Simba, Haji Manara amefunguka na kufurahishwa kurejea kundini kwa
wachezaji wake wawili ambao walikuwa majeruhi kwa kipindi kirefu na
kudai kwa kitendo hicho anaamini timu yake itashinda katika mchezo wake
dhidi ya Njombe Mji
Manara
amebainisha hayo kupitia ukurasa wake maalum mchana wa leo (Machi 29,
2018) na kuwataja wachezaji hao kuwa ni kiungo Haruna Ninyonzima pamoja
na beki Saleh Mbonde.
"Kiungo fundi Haruna na beki kitasa Salim Mbonde wamerejea kwa kasi mazoezini, timu itasafiri kwenda Njombe siku ya Jumamosi hii kupitia Iringa ambapo itaweka 'camp' hadi Jumatatu kabla ya mechi dhidi ya Njombe Mji Jumanne Aprili 3 tunaamini tutashinda inshaallah. Muhimu dua na sala zenu", amesema Manara.
Simba inaongoza katika msimamo wa ligi ikiwa na alama 46 sawa sawa na za watani wao wa Jadi Yanga huku wakiwa wanatofautiana kwa idadi ya magoli ya kufungwa na kufunga

No comments: