Yanga yafunguka juu ya Ngoma na Kamusoko
Klabu ya Mabingwa watetezi wa
Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga inatarajiwa kusafiri kesho kuelekea
Mkoani Singida wakiwa wanatokea Morogoro kwa ajili ya mchezo wao dhidi
ya Singida United mnamo Aprili mosi mchezo wao wa kombe la Shirikisho.
Hayo
yamethibitishwa na Meneja wa Yanga, Hafidhi Saleh leo (Machi 29, 2018)
na kusema programu ya mazoezi katika kambi ya timu hiyo iliyopo Morogoro
inakamilika kesho asubuhi (Ijumaa) na baada ya mazoezi wataanza safari
rasmi ya kuwafuata wapinzani wao.
"Kambi inaendelea vizuri, tunatarajia kuhitimisha mazoezi yetu siku ya Ijumaa asubuhi kisha timu itasafiri kuelekea Mkoani Singida tayari kwa mchezo. Donald Ngoma na Kamusoko wanaendelea vizuri na mazoezi kwa kufuata maelekezo ya mwalimu pamoja na benchi la ufundi kwa ujumla",amesema Saleh.
Kwa upande mwingine, Meneja Saleh amesema wachezaji wote kiujumla wanaendelea vizuri na wapo teyari kwa mchezo wao dhidi ya wapinzani wao Singida United utakaochezwa katika dimba la Namfua katika hatua ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho

No comments: