Header Ads

Wanayanga kufanyiwa ukaguzi- Mkwasa



Klabu ya Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga imetangaza siku maalumu ambayo itakutana na wanachama wake kwa lengo la kujadiliana masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo ya klabu yao.
Hayo yameelezwa na Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa mchana wa leo (Machi 29, 2018) kupitia mtandao maalum wa wanajangwani na kusema wamepanga Mei 5 kufanya mkutano huo ndani ya Jijini la Dar es Salaam
"Wanachama wa Yanga wanapaswa kufanya maandalizi ya kuhudhuria mkutano huo sasa kwa kulipa ada zao mapema kwa sababu kwenye mkutano huo ukaguzi mkubwa utafanyika kabla ya watu kuingia ndani ya ukumbi. Wanachama wenye kadi aina zote mbili wataruhusiwa kuingia ukumbuni, kwa maana ya wale wenye kadi za zamani na hizi zinazotolewa sasa kupitia benki ya posta", amesema Mkwasa.
Kwa upande mwingine, Mkwasa amesema kupitia kikao cha kamati ya utendaji kilichofanyika siku ya Jumapili iliyopita, kamati imeridhia kufanyika kwa Mkutano huo, na kuomba wanachama kujindaa kwa ajenda ambazo zitatangazwa hapo baadae.

No comments:

Powered by Blogger.