Header Ads

ziara ya Waziri mkuu wa Israel

Waziri mkuu wa Israel asema ziara yake nchini Marekani inalenga kuondoa tishio la Iran
Waziri mkuu wa Israel Bw. Benjamin Netanyahu amesema kuondoa tishio la Iran ni lengo la pamoja la Israel na nchi nyingine za Mashariki ya Kati.
Bw. Netanyahu amesema hayo kabla ya kuwasili Marekani kwa ziara ya wiki moja, na kuongeza kwamba atajadiliana na Rais Donald Trump wa Marekani kuhusu masuala mbalimbali yanayoihusu Iran, ikiwa ni pamoja na makubaliano ya nyuklia ya Iran, na vitendo vya uvamizi vya Iran kwenye mipaka ya Israel na kanda ya Masharki ya kati.
Aidha Bw. Netanyahu amesema katika taarifa yake kwamba atazungumza na rais Trump juu ya kurejesha mazungumzo ya amani kati ya Israel na Palestina.

No comments:

Powered by Blogger.