Rayvanny Aongelea Mahusiano yake Ya Kazi na Bosi wake Diamond
Msanii anaefanya vizuri na ngoma yake ya makulusa rayvanny amefunguka
na kusema kuwa ,tangu ameanza kufanya kazi na bosi wake diamond
platinumz hawajawahi kugombana au kupishana katika swala la kazi hata
mara moja.
Rayvanny anasema kuwa vitu vinavyokuwa vinatokea huwa ni vya kawaida ingawa pia vipo ambavyo huonekana kutopendezwa navyo lakini haijawahi kutokea wakagombana kabisa na kushindwa kuelewana.
Nikikosea lazima anikoromee, lakini kunikoromea hajawahi kwa sababu yeye sio mtu wa kufoka foka lakini ikitokea umekosea lazima atakwambia na utajua kuwa kitu hicho hajakipenda kwaio mtu mwenyewe hapo inabidi tu ujiongeze.-Akifunguka Rayvanny alipokuwa akiongea na funiko base ya Radio Five.

No comments: