Aliyeingia na bastola uwanjani akiona
Tukio hilo la Savvidis kuingia na Bastola uwanjani lilitokea Machi 12 mwaka huu ambapo mmiliki huyo wa PAOK alikuwa akijaribu kupinga maamuzi ya mwamuzi ambaye alikataa goli lao la dakika za lala salama dhidi ya AEK Athens.
Baada ya maamuzi hayo sasa AEK Athens ambao ni vinara wa ligi kuu nchini humo wamezawadiwa ushindi wa goli 3-0 kufuatia mechi hiyo kuvunjika. Pia PAOK watacheza mechi zao 3 zijazo za nyumbani bila ya mashabiki na wataanza msimu ujao wakiwa wamepunguziwa pointi 2.
Ligi kuu ya Ugiriki itaendelea tena wiki hii baada ya kusimama tangu Machi 12, siku ambayo vurugu hizo zilitokee.
No comments: