Askofu Manase: Kila Kanisa Likitoa Waraka Wake Taifa Halitakalika
Askofu
Mkuu wa Makanisa ya Babtisti Tanzania, Mchungaji Arnold Manase
amewataka viongozi wa dini kushauri kwa namna njema bila kutabiria nchi
mambo mabaya kwani ubaya huenea haraka kuliko wema.
Aidha, amesema kila dhehebu nchini likisimama na kutoa waraka wake taifa halitakalika.
Askofu
Manase ameyasema hayo leo Jumapili Aprili Mosi, jijini Arusha wakati
akitoa salam kwenye Ibada ya Pasaka katika Kanisa la Jerusalem Babtisti
lilipo Ngarenaro mjini Arusha.
Kupitia
Ibada hiyo, Askofu Manase amewaomba wadau wa amani nchini, ikiwamo
Serikali kukaa na wadau ili kujadili mustabali wa taifa.
“Tunahitaji kuomba amani ya Mungu itawale, kama ambavyo Yesu Kristo alivyotuachia amani yake.
“Tukiwa
kama viongozi wa dini kama kuna mambo tunaweza kushauri basi tuyashauri
kwa namna njema tusitabirie nchi mambo mabaya Kwani ubaya unaenea
haraka kuliko wema, nawasihi tuhubiri amani,” amesema Askofu Manase.
Pamoja
na mambo mengine, Askofu Manase katika Ibada hiyo ameongoza maombi
kuomba hekima kwa viongozi wa Serikali, madhehebu yote nchono ili hekima
ya Yesu Kristo ikatawale kwenye mioyo yao.
No comments: