Kinana Aongoza Viongozi Wa CCM Maombolezo Ya Winnie Madikizela Mandela
Katibu
Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana amesaini kitabu
cha maombolezo katika Ubalozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania kutokana
na kifo cha Mke wa zamani na Rais wa Afrika Kusini, Hayati Mzee Nelson
Mandela, Mama Winnie Mandela aliyefariki Aprili 2, mwaka huu.
Mama Winnie Mandela ambaye pia ni Mwanaharakati dhidi ya ubaguzi wa rangi, amefariki jijini Johannesburg, nchini Afrika Kusini akiwa na umri wa miaka 81. Mwanaharakati huyo anatarajiwa kuzikwa Aprili 14, mwaka huu.
Pamoja
na viongozi wengine wa CCM, Kinana ameongozana na Mwenyekiti wa Umoja
wa Wanawake Tanzania (UWT) Taifa Gaudensia Kabaka, Katibu wa NEC Siasa
na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI, Ngemela Lubinga, Katibu Mkuu wa Umoja wa
Wazazi, Seif Shaban Mohamed na Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM
(UVCCM), Shaka Hamdu Shaka.

No comments: