Spika Ndugai Asimulia Alivyopigania Uhai Wake
Spika
wa Bunge Job Ndugai amesimulia jinsi alivyopigania uhai wake wakati
akiwa amelazwa nchini India ambapo amesema kuna kipindi alikuwa akihisi
hawezi kuiona kesho.
Spika
ameyasema hayo bungeni leo ambapo ameongoza kikao kwa mara ya kwanza
mwaka huu tangu arejee, mara baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali
na majibu.
“Kuna
wakati nilikuwa nikiona kabisa siwezi kuiona kesho, baadhi yenu labda
hamjawahi kulazwa hospitali mkiwa mnaumwa sana na kama ukiwa peke yako,
halafu ukaona jinsi ambavyo mawazo yanavyokuja na kuzunguka na wakati
mwingine kunakuwa na dalili zinaonesha kama vile kesho hakuwezi
kukucha.”
Spika
Ndugai amesema kuna raha na tabu yake kidogo ambapo hawaombei wabunge
hao wapitie katika mambo hayo huku akiwaombea wasipate machungu hayo
aliyoyapata ambapo pia amewashukuru wale wote waliomuombea wakati akiwa
mgonjwa.
“Niwashukuru
wote walioniombea kwani binadamu siyo jiwe lazima kupita katika mapito
na kila binadamu ana mapito ambayo anaweza kupitia kulingana na
alivyopangiwa.
“Kwa
hiyo ukipata msalaba unaubeba kwa amani ninaendelea kumuomba Mwenyezi
Mungu msalaba wangu na mimi usiwe mzito sana uwe wa kadri tu.
“Vinginevyo
nashukuru tumerudi tupo pamoja na niwashukuru sana wasaidizi wangu hapa
mezani Naibu Dk. Tulia( Akson) Chenge (Andrew) Najma (Giga) Zungu
(Musa) Katibu na timu yake pamoja na wabunge kwa kipekee kabisa
Wapigakura wangu wa Kongwa, nawaomba tuendeleze gurudumu letu.
“Kipekee
nimeshukuru Waziri Mkuu, (Kassim Majaliwa), tulikuwa tunawasiliana
kipekee alikuwa akinitia moyo sana nilipokuwa kitandani kule,” amesema
Spika Ndugai.

No comments: