Ni Marufuku Kuoa bila taarifa
SERIKALI
ya Kijiji na Kata ya Nsalala Tarafa ya Itwangi Shinyanga Vijijini,
imetunga sheria ya kutokomeza mimba na ndoa za utotoni, kwa kumtaka
mwananchi anayetaka kuoa ama kuozesha kutoa taarifa kwa uongozi wa
kijiji.
Lengo la marufuku hiyo ni ili kijiridhisha kama anayeolewa siyo mwanafunzi au msishana chini ya umri wa miaka 18.
Hayo
yalibainishwa mwishoni mwa wiki na Mwenyekiti wa Kijiji cha Nsalala,
Sandeko Machungo, kwenye mdahalo wa kutoa elimu ya kupinga ukatili wa
kijinsia ndani ya jamii kupitia mitandao ya kijamii, ulioandaliwa na
Shirika la Kivulini linalotetea haki za watoto na wanawake kwa ufadhiri
wa shirika la OXFAM la Uingereza.
Alisema
viongozi wa Serikali ya kijiji mara baada ya kupata elimu ya ukatili wa
kijinsia kupitia mashirika mbalimbali, wameona ni vyema wakatunga
sheria ndogo kijijini ya kuzuia wananchi kuoa amakuozesha bila ya kutoa
taarifa kwenye uongozi huo kwa lengo la kutokomeza tatizo la mimba na
ndoa za utotoni.
“Kwenye
kijiji changu tumetunga sheria, hakuna mwananchi kuoa ama kuozesha bila
ya kuuona uongozi wa kijiji, tutafuatilia taarifa za mtu anayetaka
kuolewa kama hayupo chini ya umri wa miaka 18 na siyo mwanafunzi, kwa
kuangalia cheti cha kuzaliwa ama kadi ya klinini ndipo tunatoa ruhusa,”
alisema Machungo.
Aliongeza
sheria hiyo waliitunga mwaka jana na wananchi wamekuwa wakifanya hivyo,
na tangu ianze kufanyakazi hakuna changamoto tena ya ndoa za utotoni
kijiji humo wala mimba kwa wanafunzi.
Kwa
mujibu wa Machungo, kila mwananchi amekuwa mlinzi wa mwezake na atakaye
bainika kwenda kinyumena sheria hiyo kijiji kitamshughulikia.
No comments: