Azam FC yakusudia kuipoteza Yanga SC
Uongozi wa Klabu Bingwa ya
Afrika Mashariki na Kati, Azam FC umefunguka na kudai watatumia ipasavyo
mchezo wa mwisho dhidi ya Yanga ili waweze kuchukua ushindi wa nafasi
ya pili ambayo kwa sasa ndio nafasi pekee iliyobakia inaangaliwa kwa
vilabu hivyo.
"Tumeuchukulia mchezo huu kwa uzito mkubwa sana kwa maana tunataka ushindi wa nafasi ya pili lakini nafasi hiyo hatuwezi kuipata kama hatutofanya vizuri katika mechi ambazo zipo usoni kwetu. Yanga kiukweli hawakuwa na matokeo mazuri katika kipindi hiki kwa maana mechi zake za mwisho imekuwa inapoteza poteza lakini Azam FC haitakuja kwenye sura ile ambayo watu wanaiona sasa hivi", amesema Maganga.

No comments: