Rais wa Jamhuri ya muungano
wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa mwenyekiti wa
Bodi ya wakurugenzi ya chai Tanzania (TBT) na Mkurugenzi wa Taasisi ya
Utafiti wa kilimo Tanzania (TARI).
Katika
taarifa ilitolewa na Ofisi ya Kurugenzi Mawasiliano Ikulu leo Mei 23,
2018 imeeleza kuwa Mhandisi Steven Daudi Mlote, ameteuliwa kuwa
mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya chai Tanzania (TBT) na kuongeza
kuwa Mhandisi Mlote anachukua nafasi iliyoachwa wazi na mtangulizi wake
Mh. Anne Makinda ambae amemaliza muda wake.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo imeongeza kwamba uteuzi wa Mhandisi Mlote ulianza Mei 21, 2018.
Sambamba na hayo Rais Dkt John Magufuli amemteua Dkt. Geofrey Mkamilo
kuwa Mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa kilimo Tanzania (TARI),
uteuzi wake umeanza Mei 22, 2018 na anachukua nafasi ya Dkt. Fidelis
Angelo Myaka ambaye amestaafu.
No comments: