
Mwanamuziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz amefunguka na kuuanika
ukweli wazi kabisa kuwa Nillan ni mtoto wake na sio mtoto wa Marehemu
Ivan Semwanga kama wengi wanavyodai. Kwa muda mrefu kumekuwa na tetesi
zinazodai kuwa Nillan sio mtoto wa Diamond ambapo ilidaiwa kuwa Zari
alichepuka na Ivan kipindi yuko na Diamond ndio akamzaa Nillan. Diamond
ameamua kuzima kabisa tetesi hizo na kuanika kuwa Nillan ni mtoto wake
na kuwataka mashabiki wasilete uchonganishi Kwenye familia yake hasa kwa
wanaye. Siku ya jana Mama Diamond aliposti picha ya Baba Diamond akiwa
amembeba Diamond wakati mdogo na Diamond alikomenti kwenye picha hiyo
kuwa anataka aonganishe picha hiyo na ya Nillan ili watu waone jinsi
walivyofanana na kuacha kusema yule sio mtoto wake. Dah hii picha
nilikuwa naitafuta sana…kuna picha moja nimembeba Nillan kama hivyo
nilikuwa nazimix niwawekee maboya wanaokazana kusema Nillan sio
mwanangu…mxiew”. Lakini pia Diamond alimtolea povu zito shabiki na kumta
asimgombanishe na watoto wake: Usiniletee uchanganishi na matimu yenu
kwa wanangu…watoto wote ni wangu Tiffah, Nillan, Dylan… hivyo yaani”.
No comments: