Mwanadada mchekeshaji kutoka timamu Ebitoke ameweka siri ya
mafanikio yake katika kazi na kusema kuwa tabia yake ya kipekee na
ubunifu wa kupaka wanja wa kuukoleza ndio uliompa kazi, jina na ajira
katika tasnia ya maigizo. Ebitoke anasea kuwa yeye hawezi kufanya make
up kama watu wengine wanapokuwa katika lication kwa sababu wanja ndio
kitambulisho chake kikubwa katika kazi yake, na kusem akuwa endapo
atabadilisha aina ya kujiremba na kuanza kupaka tofauti basi
atasahaulika kabisa. Ninauheshimu sana wanja kwa sababu ndio ulionipa
maisha ,hata akaunti yangu ya benki inafanya vizuri sana na nimetimiza
ndoto zangu nyingi tu kwasababu ya huu wanja ingawa watu watakuwa
hawauelewi.
No comments: