Header Ads

Irene Akai peke yake , Anaogopa Kutokewa na Mzimu wa Masogange


Mwanadada Irene Uwoya ameweka wazi kuwa muda mwingi tngu kufariki kwa aliyekuwa rafiki yake kipenzi agness masogange amekuwa akiogopa kukaa peke yake kwa sababu anahisi kama mzimu wa rafiki yake huyo unaweza kumtokea. Irene Uwoya ansema kuwa kwa jinsi alivyokuwa karibu na rafiki yake Agness Masogange imekuwa ngumu sana kwake kukaa peke yake na ndio maana hata baada ya msiba ilikuwa ngumu kwake kuendelea kukaa katika nyumba iliyokuwa karibu na nyumba ya aAgness na kubidi ahame . Nahofia sana kutokewa na agness jamani,yaani imekuwa ni lazima niw mtu wa kujichanganya kila siku  ili nisiwe ninamkumbuka na mambo mengi yanayomhusu.Alisema Irene alipokuwa akiongea na GPL. Irene na Agness walikuwa marafiki wa muda mrefu na walikuwa wakikaa karibu karibu katika mtaa wa Makongo juu jijini Dar lakini baada ya kifo  cha masogange ilibidi irene kuhama eneo hilo ili kuepueka kumkumbuka sana  rafiki yake.

No comments:

Powered by Blogger.