Rais Magufuli akabidhi bilioni 50
Akiongea
wakati wa kikao kazi cha kuanza ujenzi wa miundombinu hiyo kwa wilaya
zote sita Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe.Paul Makonda amesema fedha
hizo ni za serikali kutoka kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwaajili ya
ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo lengo likiwa nikuziwezesha
kuwa na miradi itakayozalisha fedha na kujitegemea ili kutoka kwenye
utegemezi.
Aidha, Makonda amesema fedha hizo hazina riba ni mbadala wa fedha za maendeleo kutoka kwa wahisani ambao huwa wanatoa riba za kiwango kikubwa hali inayopelekea taifa kuwa na deni kubwa nje ya nchi.
Kuhusu ujenzi wa kituo kipya kikubwa cha uwekezaji cha Afrika Mashariki ambacho kinatarajia kujengwa ilipo stendi ya mabasi makubwa kwa sasa Ubungo Bus Terminal amesema wapo katika hatua nzuri kimchakato.
Miradi itakayotekelezwa na fedha hizo ni Kituo cha kimataifa cha mabasi makubwa ya abiria ya ndani na nje ya nchi kitakachojengwa Mbezi Luis, soko kubwa la Kisasa eneo la Kisutu,machinjio ya kisasa Vingunguti,madaraja,barabara na hospitali.

No comments: